UKIMWI nchini Afrika Kusini

VVU / UKIMWI nchini Afrika Kusini ni gonjwa mojawapo lenye kuleta wasiwasi mkubwa kiafya . Nchi hiyo ina idadi kubwa zaidi ya watu wanaougua VVU kuliko nchi yoyote barani Afrika na ina kiwango cha nne cha juu cha maambukizi ya VVU, kulingana na takwimu za 2019.[1] za Umoja wa Mataifa.

Kulingana na hifadhidata ya UNAIDS iliyoangaziwa kutoka Benki ya Dunia, mnamo mwaka 2019 kiwango cha maambukizi ya VVU kwa watu wazima wenye umri wa miaka 15 hadi 49 kilikuwa asilimia 37 huko Eswatini (Swaziland), asilimia 25 nchini Lesotho, asilimia 25 nchini Botswana na asilimia 19 nchini Afrika Kusini.[2]

  1. "World Development Indicators | DataBank". databank.worldbank.org. Iliwekwa mnamo 2021-08-17.
  2. "World Development Indicators | DataBank". databank.worldbank.org. Iliwekwa mnamo 2021-08-17.

© MMXXIII Rich X Search. We shall prevail. All rights reserved. Rich X Search